Home AUDIO “Chagueni Presenters wenye wanaelewa mziki kulingana na kipindi,” Dully Sykes aliskika akiongea...

“Chagueni Presenters wenye wanaelewa mziki kulingana na kipindi,” Dully Sykes aliskika akiongea off-mic – Sunsetkenya

Imekua wiki nzito kwa watangazaji wawili wa kituo cha Pwani Fm baada ya ile interview ilioleta maneno kibao mitandaoni. Mgeni alionekana akifunika wenyeji wake kwa kutupia facts kwa kile alichoamini hakifanywi sawa.

Kwa interview hio, Dully alikemea vikali vitendo vya wendeshaji vipindi mjini Mombasa kwa kutekeleza kilicho chao na kushabikia cha jirani. Dully aliamini mafanikio ya wasanii wa nyumbani yako kwa mikono ya presenters na Djs wa nyumbani.

Gumzo ilizuka pale mtangazaji aliskika akisema wasanii wa nyumbani hawaimbi vitu za kueleweka. Gumzo hilo lilimkasirisha sana Dully kisha mashabiki wakapandwa na gadab kubwa kisha mijadala tofauti kusuta tamko hilo ikazuja mitandaoni. Wengine wakiomba kuachishwa kazi kwa watangaji hao, wengine wakiwaomba watangazaji hao kuomba msamaha kwa hadhira kwa kuwakosea sana wasanii wa pwani.

Kilicho vutia zaidi ni pale Dully Sykes aliskika akisema “Chagueni Presenters wenye wanaelewa mziki kulingana na kipindi,” Jambo ambalo lilileta muhemko mkubwa ndani ya studio za pwani fm.

Nilipata nafasi ya kuongea na mashabiki kuwauliza mawili matatu na wengi walikua na haya yakusema, “Alaf sasa before interview mtu unafanya research ya kutosha on the subject.. Sasa mtu Hujui ata anisa iliimbwa na Nani, Hujui wasanii wa likoni na nyimbo zao. Hujui nyambizi na msanii uko nae apo nkama hukufanya research. Very wrong.

Shabiki mwengine naye akasema haya, “Bro Pwani Fm naijua vizuri sana nje ndani nishawai kuwa hapo, Maximillah namjua vizuri sana enzi Aisha Sagaf ndio Mdosi apo mi niingia kibahati kutoka Nairobi na amini usiamini sikutoboa kwa sababu yakujuana… infact Sagaaf aliporudi nairobi Maximillah akachukua uongozi akiwa nikajikuta niko nje nikatoka nikahamia Radio rahma 2009, so naelewa sana mambo ya ukabila nakujuana…. Pwani fm ilikufa wakati Peter Adamz, Sagaf na Donde Samora walitoka hapo, nashkuru nilipata fursa yakufanya nao kazi……. enzi hizo pwani fm ilikua ina compete na baraka fm sahii zote zimebaki majina tu hazina impact tena kwa jamii.”

Hiyo iliisha nakina Donde Samora, Peter Adamz, Dj Lenium, Tom Japanni… hizo enzi ndio ungefurahia mziki wa mombasani.”

Je vipi kuhusu presenters wakongwe Pwani fm kama vile Munga? Shabiki alikua na haya yakusema,”Siezi shangaa kabisa, Mafimbo nae alikua serious wakati kina donde na peter adamz wako alikua anawapa compe lakini tangu abakie pekeyake yuko tu stagnant tu utadhani ndio ameajiriwa leo na ako na zaidi ya miaka kumi hapo, sahii inafaa awe ameshika mbaya lakini unakuta ma new comers wa radio kaya wako na impact kumliko.

My advice to them, kindly do some good research before your guest knocks you down.

Previous articleNaiboi and Avril squash beef with double video release – Sunsetkenya
Next articleMIXTAPE | Dj MarcusVado – Mzuka Kibao Mix vol 9 – Sunsetkenya

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here