Home GOSSIP Hivi unajua Naona Bado yake Sudi Boy iliandikwa na Tee Hits?

Hivi unajua Naona Bado yake Sudi Boy iliandikwa na Tee Hits?

Ni takriban miaka mitano tangu wimbo wake Sudi Boy akimshirikisha Ameleena kutoka kwa jina Naona Bado.

Ni wimbo uliopata mapokezi mazuri kwani uliskika kila Kona ya mtaa hadi ukawa wimbo Bora wa mwaka.

Watoto kwa wazee walionekana wakifirahia utunzi huo kwani kila mtu ama kila rika lilionekana likifurahia wimbo huo kwa ustadhi wa mashairi yake na utunzi ulio bora.

Msanii Sudi Boy

Sudi Boy akiwa Msanii alichipuka na kukubalika kwa miondoko yake ya kuimba. Wengi walimjua kwa wimbo wake Banati uliomtoa na kumtambulisha kwenye Sanaa ya Mziki huku akijizolea lukuki wa mashabiki.

TETESI.

Habari zinazotufikia ni kwamba wimbo wake Sudi Boy na Ameleena ulikumbwa na tafaruku kwani TETESI zinasema, originality ya wimbo uliandikwa na kutayarishwa kwa mara ya kwanza na Producer Tee Hits kabla ya Msanii Sudi Boy kuhamia Grandpa Records kwa Refigah.

Kutua kwa Sudi Grandpa kulimpa azma na hamu ya kutengeza wimbo huo tena ndani ya studio za Grandpa.

Mazungumzo ya Sunset Kenya na producer Tee yalivumbua mengi yalio ibuka enzi zile mpaka kufikia kiwango cha kuletea wawili hao uhadui.

Hebu tizama kile Tee alichozungumza hapa:

Producer Tee Hits.

Nakumbuka 2014 December Sudi alikuja kwangu so ile kutulia studio ndio tukapata idea ya wimbo “Naona Bado” nikaunda beat na kuanza kuandika mistari shahidi ni Mafimbo alikua so wimbo ukakamilika…

Wakati tunapanga kuutoa jamaa kaenda Nairobi Grandpa akaurudia wimbo huo bila ruhusa yangu… So mimi kumuliza ni vipi jamaa alinileta juu akakataa kabisa hata split sheet…

Kilichoniuma zaidi ni aliulizwa vipi mwenye aliunda hii idea ya kwanza tunamlipa vipi akasema aah ni producer kanjanja tu huko Mombasa hana nouma… Nikamuliza kibinadamu ni vipi akanijibu eti sina uwezo wakufanya hit na kama kweli hyo Naona bado ni mimi nimeandika basi nifanye hit ingine…

Nikamwambia sawa na yeye kama ndio aliandika Naona Bado basi afanye ingine yenye itapita hyo…. Mpaka leo Sudi anatapatapa mimi after hapo ndio nikaunda Kidekide ikahit Kenya Nzima na Nchi zengine.. Moral of the Story, Wasanii Laana zengine mnajifakia alaf mnasema mumerogwa.

Unaweza kupakua NAONA BADO audio hapa Kisha upate utamu zaidi.

Unaeza tizama Video ya NAONA BADO Hapa;

https://youtu.be/kg6vslnx-Pw

Previous articleMIXTAPE | The Great Infinity (22 Djs) Vol 15 – Gengetone & Bongo Mix 2022 [Mp3 Download]
Next articleVIDEO | Kata – Beka The Boy [Mp3 Download]