Home TRENDING Kimaajabu Vile! Gari la Kubebea Maiti Lawaka Moto Mwili Ukiwa Ndani

Kimaajabu Vile! Gari la Kubebea Maiti Lawaka Moto Mwili Ukiwa Ndani

Kama umeyaona yote dunia basi hili litakushangaza.

Gari moja la kubebea maiti limewaka moto huku mwili wa mwendazake ukiwa ndani ya gari hilo huko nchini Afrika Kusini.

Ilibidi wazima moto kuingilia kati mkasa huo ambao waliweza kuokoa mwili kwa juhudi kubwa sana huku gari na sanduku la kubebea maiti zikiteketea sana.

Mkasa huu ulitokea msafara ukiwa njiani kuelekea kwa wanafamilia ili kutizama na kupeana heshima yao ya mwisho kwa mwenda zake.

Kabla ya kuaga, mzee alikua na bibi wawili ambao inaripotiwa walikua na mvutano kila mmoja akitaka kumzika bwanake kwa boma yake, kwani imethaminika wote wawili (bibi) walikua na boma mbali mbali.

Kulingana na ripoti, chanzo cha moto bado hakijajulikana. Bado uchunguzi unaendelea.

Previous articleVIDEO | PASCOLE – MI NAWE | MP3 DOWNLOAD
Next articleVIDEO | Pamoja Tunasonga Mbele – Coast Artistes | Mp3 Download