Home ENTERTAINMENT Lava Lava Amwaga Machozi Baada Mpenzi Wake Kukataa Msamaha Dharani

Lava Lava Amwaga Machozi Baada Mpenzi Wake Kukataa Msamaha Dharani

0

Imekua ni kawaida mastaa wengi kuchukua fursa ya kuwavamia wapenzi wao hadharani kuwaomba msamaha baada ya labda kukosana ama hata pale wapoenda kombo.

Hivyo basi, Msanii Lava Lava aliweza kuvamia studio za wasafi fm akiwa amebeba maua ili kumzawadi na kumuomba msamaha mpenzi wake Lulu Diva, ila kilichomtokea asilani hatasahau maishani mwake.

Kipande cha video kilichovuja kinamuonesha msanii huyo akienda chini kwa magoti na kumuomba Msamahe Lulu Diva ila, Diva alichukua maua hayo na kuyatupa chini mbele ya wapiga picha kisha kumsukuma mbali Lava Lava kabla ya kutoka studioni humo.

Aliskika Lulu akisema iwapo angejua mwaliko huo ungemleta Lava Lava basi katu hangeitikia mwaliko huo.

Kwa kweli ni tukio lakudhalilisha na pia kuumiza moyo.

Je, uko na yapi yakuwaambia wapenzi hao wawili? Angusha komenti yako.