Home ENTERTAINMENT NGOMA KUTAMBAA TENA KATI YA CHIKUZEE NA SUSUMILA!!

NGOMA KUTAMBAA TENA KATI YA CHIKUZEE NA SUSUMILA!!

0

Utata wa mda mrefu kati ya nguli wawili wa hitsongs kutoka pwani Susumila na Chikuzee unaonekana kuyeyuka!

Hii ni baada ya ukaribu wa wawili hawa kuzidi kuonekana kila uchao na tayari mioyo ya mashabiki wao iliokua na kiu ya zaidi ya miaka sita kuanza kugeuza mapigo ya matumaini ya kukatwa kiu hio.

Pia, Soma Mzee aaga baada ya kubugia Viagra kisha kukosa Mnofu Migori.

Ikumbukwe wawili hawa wamesemekana kwa mda mrefu kua na ugomvi kuanzia mapema mwaka 2015 baada ya ngoma zao “Ngoma itambae” na “Hidaya” kuchafua anga na kueka rekodi ya nyimbo zilizochezwa sana kutoka mkoani pwani, rekodi ambayo bado wasanii wengine wamekosa usingizi kuivunja!

Mda wa nyuma walitupia picha mitandaoni iliojumuisha wasanii wenza Dazlah, Ali B na P day na kuzua gumzo kiasi cha haja.

Pia, Soma Njoo Niliyofanya na Sho Madjozi imenifanya niwe na maongezi na Producer wa Davido.

Ati ati za wasanii hawa kuandaa Jiwe lingine zimepigwa jeki baada ya wao kuonekana kwa video fupi wakipiga mzaha wa kicheshi studioni huku Susumila, anaepeperusha angani bendera ya 001 Music akisikika kumtania Abdhallah Chikuku, ambae mda mfupi baadae aliitwa kumalizia ‘line’ yake kwenye ‘beat’ iliokua ikiendelea.

Kwa sasa Susumila anaendelea kufanya vizuri na E.P yake ya ‘King is King’ baada ya collabo yake na malkia wa Amapiano Sho Madjozi kutoka South Africa kurushwa mawe na baadhi ya mashabiki.

Pia, Soma Kumekuchaaa! RAYVANNY Amvua nguo HARMONIZE “Umemtumia PICHA za UTUPU PAULA Wewe ni MTU wa aina gani?”

Je, endapo wawili hawa watafanikiwa kufumua hit song ingine, unadhani itaamsha tena mziki wa pwani unao onekana kuyumba?

Wazungu husema ‘fingers crossed’ wacha tutegee tone la maji baridi jangwani.

Kheri Prince
Mwandishi

Facebook Comments Box