Home ENTERTAINMENT Nitafanya kazi na kila mtu. Lazima niwahoji Harmonize, Alikiba na Ommy Dimpoz...

Nitafanya kazi na kila mtu. Lazima niwahoji Harmonize, Alikiba na Ommy Dimpoz ndani ya Wasafi Fm, asema Lil Ommy – Sunsetkenya

0

Kuhamia kwa mtangazaji Lil Ommy Wasafi kumeleta taswira mpya kwenye tasnia ya mziki nchini Tanzania.

Ikumbukwe Ali Kiba nimhasimu mkubwa sana wa Diamond na hajawahi kukanyaga kwenye office za Wasafi Media. Sasa ujio wa Tambwe kwenye Station hio ya redio kumefungua milango mingine tofauti.

Alipoulizwa iwapo atatumia mbinu gani kuwaleta wasanii hao kwa mahojiano, nguli huyo aliapa kutumia fursa hio kama alivyoajiriwa nakuleta mahasimu hao karibu ili kuzidi kupeleka tasnia ya mziki nchini humo mbele zaidi mbali na pale wako kwa sasa.

“Nitajaribu kumaliza tofauti hizo ili mziki wetu uweze kufikia nafasi za juu zaidi. Nachukua nafasi hii si kwakua nimejiunga na wasafi hapana, Wasafi Media iko na utaratibu wake mbali sana na Wasafi Records. Nitafanya kazi kama ilivyokua mbeleni. Hakuna mabadiliko kwa mipangilio yangu. Mimi ni mtangazaji mwenye busara na uelewa kwa mambo ninayo fanya,” Alisema mtangazaji huyo.

Haya tutarajia kumuona King Kiba Wasafi Fm wakati wowote ule manake nguli ametuhakikishia hilo litakamilika.

Facebook Comments Box

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here