Home HEALTH Ukuzaji wa bangi Igembe, Meru

Ukuzaji wa bangi Igembe, Meru

0

Wapo wanaohofia na kujali maisha yao ya kesho ila katika kijiji cha Thuuru Igembe Kaskazini Kaunti ya Meru kisa ni tofauti kwa jamaa anayejulikana Kama M’mwambia ambaye ametiwa mbaroni kwa kukuza na kufanya boma lake kituo cha kutengenezea na kusafirishia bangi.

Wakaaji wa eneo hili wanalalamikia kile wanasema kwamba watoto wengi haswa wasichana waliacha shule, afya kudhohofika, wazazi kuharibika na wengine kuwa vichaa sababu ya utumizi wa bangi.

Katika mawasiliano na mkuu wa kijiji cha Thuuru ,jamaa huyu amesema kwamba amefanya kazi hii kwa zaidi ya miaka kumi na ana kundi ambalo huja kuchukua na kusafirisha bangi katika mitaa tofauti tofauti.

Walipofululiza hadi shambani wakapatana na maajabu kwamba jamaa kapalilia vizuri bangi sehemu kubwa sana katika shamba lake.

M’mwambia pamoja na watu wengine walikamatwa huku wengine wakitoroka wasijulikane walipo. Polisi wanawasaka waliotoroka.

Facebook Comments Box